Page:Swahili tales.djvu/446

This page has been proofread.
426
NYANI, NA SIMBA, NA NYOKA.

kwanza alipokwenda mitegoni, ameguiwa nyani. Akataka kuliwaga. Lile nyani likasema, Ewe bin Adamu, usiniwage, njoo ninamue katika mtego, niponya kwa mvua, nije nikuponye kwa jua. Alipokwisha namua nyani, likasema, nakupa wasia wangu bin Adamu si mwema, usimtende mema, ukifanya, kesho atakuja kufanya viovu.

Hatima akaja siku ya pili, katika kuonja mitego, ameguiwa nyoka. Akapiga mbio kuita watu mjini. Akasema nyoka, Rudi, bin Adamu, usiende mbio mjini, usiende kuniitia wakaja niua, nifae katika huu mtego, nami kesho nije nikufale, lakini bin Adamu hafanyii mema mtu.

Siku ya tatu akaenda kuonja mitego, akafika mtegoni, ameguiwa simba ni mtego. Bin Adamu yule mwenyi mtego, akamwona mzee simba akamatwa ni mtego, akapiga mbio kwenda kuita watu kuja 'mua. Simba akamwambia, La; niponya wa mvua, na nije nikuponye ya jua. Illakini alipokwisha namua katika mtego, yule simba akamwambia, Bin Adamu, umenifaa, umenitenda mema, illakini wasia wangu nakusia, Binadamu hafanyi mema. Siku ngine mtu ameguiwa ni mtego, yule mwenyi mtego akamnamua.

Hatima yule kijana kande zikamwishia katika nyumba zote, wakapatiwa ni njaa, yee na mamiye. Akamwambia mamiye, Mama nifanyie mikate saba. Alipokwisha kufanya mikate saba, akashika uta wakwe, akaingia mwituni kuwinda nyama, akapotea, mikate akaila sita, ikaisha, ukasalia mmoja.

Uliposalia ule mmoja, akaenenda hatta mwituni mwitu