Page:Swahili tales.djvu/452

This page has been proofread.
432
NYANI, NA SIMBA, NA NYOKA.

Akaenda mtu kumtwaa yule mgeni, akaja naye na mkoba wakwe. Ukafunguliwa ule mkoba na watu tele wakashuhudia vyombo vya mwana wa Sultani, wakashuhudia tena na vyombo vya watoto wa Waziri, na watu mjini. Hatima akafungwa mikono nyuma kwa kamba.

Ile joka likatoka kisimani, likija hatta mjini. Akazunguka mji, akasimama panapo yule bin Adamu. Watu wakataharruki katika mji hatta wakasema na yule bin Adamu, wakamwambia, sema na huyu nyoka, ende zako. Nyoka yule akaja. Watu wakamfungua yule bin Adamu mikono nyuma aliofungwa. Nyoka yule akarudia kisimani kwakwe, akamwambia, Ewe bin Adamu, kadri utakapofanywa maovu, nipigia ukemi, nami 'takutokea marra.

Naye akapata heshima katika inchi. Akaulizwa, kwani wee huyu kuwa mwenyeji wako, akakufanya maovu? Akawaambia, katika nyoka, na simba, na nyani, walinambia kwamba bin Adamu hafanywi mema, ukimtenda mema bin Adamu yee hukutenda maovu, nayo ni kweli wala si uwongo. Yule mema niliomtenda naye anifanya maovu, ule wasia wa nyoka na simba na nyani ni kweli, wala si uwongo.

Sultani akauza maana yakwe, akamweleza yalivyokwenda. Sultani akasema, huyu yastahili kutiwa katika fumba akatoswa baharini, kwani hajui mema, yee amefanywa mema, amelipa maovu.