Page:Swahili tales.djvu/464

This page has been proofread.
444
HADITHI YA LIONGO.

niteleze kama nyoka, nipande madari na kuta, nikitezama huko na huko.

Akamwambia, salaam sana mama, mwambie kama haya niliokwambia. Akaenda, akamwambia mamaye, akamwambia, salaam sana mwanao, ameniambia maneno kuja kukwambia. Akamwambia, maneno gani? Akamwambia, kama yale yalioambiwa.

Mamaye akajua, akaenda zake dukani, akabadili mtama, akampa mtumwa wake kutwanga. Yeye akaenda kununua tupa nyingi, akaleta. Akatwaa unga ule, akafanya mikate mizuri mingi. Akatwaa chachu, akafanya mkate mkubwa, akatwaa tupa akatia ndani, akampa mtumwa wake, kumpelekea.

Akaenda nao, akifilia mlangoni asikari wakamnyang'anya, wakachegua mikate mizuri, wakala wao. Ule wa chachu wakamwambia, mpelekea bwana wako. Yule akampelekea, akauvunja, akatoa tupa zile akaziweka, akala mkate huu akanywa maji, akashukuru Muungu.

Na wale watu mjini wataka auawe. Mwenyewe akasikia ya kuwa ya kwamba utauawa. Akawaambia asikari, nitauawa lini? Wakamwambia, kesho. Akawaambia, kanitieni mama yangu na mwenyi mji, na watu mjini wote, nije niagane nao.

Wakaenda, wakawaita, wakaja watu wengi wote, na mama yake na yule mtumwa wake.

Akawauliza, mmekutanika nyote? Wakamjibu, tumekutanika. Akawaambia, nataka pembe, na matoazi, na upato, zikaenda zikatwaliwa. Akawaambia, nna machezo leo nataka kuagana nanyi. Wakamwambia, vema, haya,