Page:Swahili tales.djvu/472

This page has been proofread.
452
HADITHI YA LIONGO.

Wakamwita mamaye, wakamwambia, enenda kasema naye mwanao, aondoke, tupate maji, ao tutakuua wewe.

Akaenda hatta alipofika akamshika mwanawe kumtumbuiza kwa nyimbo, akaanguka. Mamaye akalia, akajua mwanawe amekufa.

Akaenda kuwaambia watu mjini, ya kwamba amekufa, wakaenda kumtezama, wakamwona amekufa, wakamzika, na kaburi lake laonekana katika Ozi hatta leo.

Wakamkamata kile kijana, waka'mua, wasimpe ufaume.