Page:Swahili tales.djvu/476

This page has been proofread.


MASHAIRI YA LIONGO.


Nabudi kawafi takhamisi kidiriji,
Niwathihishe izagale kama siraji,
Ili kufuasa ya Liongo simba wa miji.

Ai wanji wanji nazawanji kisiza wanji; ma kadiliza kasiliza, mwanangwa mema.


Pindi uonapo ali shari mume mwendo,
Pindua mtima nutie kani na vindo,
Uwe ja namire, tui mke, katika shindo.

Mwanangwa mbonaye mbuzi wako katika mwendo; uki­metwa pembe na mkami akimkamaa.


Akhi ewe mbuya twambe mambo ya kujelele,
Huyu muungwana shati ’ari haiondole,
Nakuchea kufa mwenyi cheo kavilikele.

Mwanangwa mbonaje muhakara wakwe wiimile; asirathi kufa na mayuta yakaya nyuma.




The same in ordinary Swahili.

Nandiliza ushairi wa utanu nikipita kwa upesi,
Nipambanue utoe nuru kama taa,
Kwa ajili kufuata Liongo simba wa miji.

Ee ungi ungi naanza kwa wengi; pamoja na ukiandaliza nikaishiliza kizao cha mambo mema.


Pindi ukiona mwenyi ubaya mume mwenziwo,
Geuza moyo uvike bidii na machungu,
Iwe kama chui, chui mke, katika kundi.