Page:Swahili tales.djvu/48

This page has been proofread.
28
SULTANI DARAI.

mume atoka amwulize mkewe. Je! bibi, umepika? Je! bibi, watoto wamekula? Je! bibi, chakula ulichowapa watoto kimewatosha?

Bassi nami mke ndio nikujibupo. Ah! Bwana, watoto chakula kimetosha. Ndipo watu wanapokaa na wake wao katika majumba, ndipo watu wakaoa makusudi wakitoka nje wasimwulize mtumwa, wala wasimwulize mtoto, ni kuulizwa mke aliomo nyumbani, ndiyo mwenyi madaraka ya nyumba, ndio maana watu wakaoa wake kutaka haya, akija akute killa kitu nyumbani tayari. Na kitapopungua killa kitu katika nyumba asiulizwe mtumwa, wala asiulizwe mtoto, uniulize mimi mkeo, nilio katika nyumba, ukitaka kunipiga, ukitaka kunifunga, ukitaka kunitukana, ni lile ulipendalo, mume wangu, nikikosa ndilo.

Bassi, mke wangu, nisamehe kwa haya naliyofanya, wala sitafanya tena, bassi nawe, twende zetu tukalale.

Hatta usiku ulipokucha, mumewe kuondoka, akamwambia, bibi, leo mimi siendi kazini, naona maungo yote yananiuma, lakini nitaondoka marra moja, nitakwenda kwa jirani, ntakwenda kucheza bao. Bassi chakula kikiisha, mtume mtoto aje niite. Akamwambia, marahaba, mume wangu.

Mwanamke akaenda jikoni akavunja nazi. Alipokwisha pika wali jua limekuwa mafungulia ng'ombe. Mumewe hajadiriki kwenda kwitwa, amekuja mwenyewe nyumbani. Ee mke wangu umekawia mbona kupika. Nami bwana, nimekwisha kupika, lakini bwana ninakosha sahani, nalitaka kumtuma mtoto kuja kukwita, bassi, bwana,