Page:Swahili tales.djvu/52

This page has been proofread.
32
SULTANI DARAI.

jawabu hii, hili linalokuliza nami nipate kulijua. Akamwambia, sina hatta kitu, baba. Akamwambia, itayamkini kulia burre wee? Akamwambia, ninalia tu.

Mkewe akaja. Weye wafanya nini kwa mtoto? Namtezama huyu kijana, namwona akilia, namwuliza linaomliza, hanambii. Akamwambia, wataka nini na kijana, kijana huyu mpumbavu, ana wazimo, huyu amekwenda huko kwenda kwiba tango la watu, amekuja hapa, nimeliona nimemnyang'anya lile tango, nimewapa wenyewe. Bassi kijana huyu anataka kutuvumbulia vita, anataka kutujongea kutukana na watu, atatujongea kupigwa na watu, tezama huyu mtoto wangu, haendi kutwaa kitu cha watu, akiisha kula, hukaa kitako akasuka ukili wake, akichoka kusuka hulala. Huyu mtoto wako hakubali, akiisha kula kwenda ndani ya mashamba ya watu, akitwaa vitu vya watu, hutaka kutujongea sisi maskini ya Muungu. Wakija watu wenyi vitu vyao mimi simo, najitoa, nitawaambia enendeni kwa babaye, kama kulipa ulipe wewe, kama kufungwa ufungwe wewe, kama kupigwa upigwe wewe, na haya yote yatakupata kwa sababu ya mwanao, kwani mwanao hasikii, harudiki, haambiliki. Bassi mtoto huyu mtu mtendani? Bassi mimi nimejitoa, mume wangu, mimi simo kwa sababu ya vitendo vya kijana huyu.

Babaye akamshika mkono yule mtoto, akaingia naye ndani akamfunga mikono na miguu, akamchimbia na mti kati, akamwambia sikufungulii, shuti utakufa papo hapa.

Akamwambia, baba unifungie nini, wanifunga kunionea