Page:Swahili tales.djvu/58

This page has been proofread.
38
SULTANI DARAI.

mwambia, natoka nalo huko shambani kwa watu, akinyang'anya lile tango, akimpa mwanawe. Bassi mimi tena nikafanya roho yangu hasira, nikafanya roho yangu kuonewa, nikajiinamia hakumbuka mama yangu, hanena tango hili, kama ningekuwa na mama yangu, hangeweza kuninyang'anya huyu, akampa mwanawe. Nami naliogopa kumwambia, matango haya ninakwenda nikichuma kule katika kaburi ya mama yangu, angekwenda marra moja, akaenda akayachuma yote, akampa mwanawe, nami ningeyakosa. Bassi mwenyewe mimi nimeyaacha maksudi kule kaburini, nikiumwa na njaa nikapate moja nitafune, nidanganye roho yangu, na moja nifanye mtoto. Bassi mimi matango yale sikuyaiba baba, kama husadiki baba, mwenyewe enenda hatta chini ya kaburi, kuna matango saba makubwa, na madogo yaliomo na maua, hayana idadi. Bassi umenifunga, baba, kwa kunionea, sina naliolikosa kwako, wala kwa huyu mkewo.

Akamfungua mwanawe, akamwambia, mama niwie rathi kwa haya naliyokutenda, nami sikuyajua, wala sikuyasikia, wala sikuyatambua. Ah! baba yangu, mimi ni rathi kwa lo lote unitendalo. Bassi kesho, mwanangu, ntakununulia mtumwa mwanamke, na nyumba nikuhamishe, nikuweke nyumba ya marehemu mamayo, wewe na mtumwa wako, na chakula ntakupa.

Hatta usiku walipokucha, akaenda zake sokoni, jua limekuwa saa ya tatu, akazabuni mjakazi mzuri ampendaye, akampeleka nyumbani. Akamwambia, mwanangu, huyu mtumwa wako, huyu ndiye ni yaya yako, huyu ndiye mama yako, bassi nawe kaa naye. Wee Mjakazi! Lebeka, Bwana. Mimi nimekununua sababu ya mwanangu, umpikie