Page:Swahili tales.djvu/68

This page has been proofread.
48
SULTANI DARAI.

shughuli zao, hatta ussubui. Siku ya pili ile wakampelekea habari mume, Umekuwa wakati, njoo, uoe, upate kuingia nyumbani. Yule mjumbe akaenda hatta akafika kule nyumbani akamkuta yule bwana amekaa barazani, awangoja watakaomwita. Akamwambia, bwana unakwitwa, wakati umewadia. Akamwambia, mimi tayari, Ee wala.

Akaondoka yeye na jamaa zake, wakaenda, hatta wakifika katika ile nyumba ya mkwewe, akapiga hodi! Akamwambia, hód! karibu Shekh, karibu na wangwana. Akamwambia, tumekaa. Wakapita barazani, wakaenda, wakaita mwalimu. Akaja akawaoza. Kwa kuondoka wale watu wakapewa wali, wakala, wakafanywa na uzuri sana, wakaambiwa, wangwana karibuni. Wakamwambia, na wewe, bwana harrusi, kua heri. Wakatoka, wakaenda zao.

Akaingia ndani katika nyumba yake, wakakaa katika nyumba ile ya mkwewe muda wa siku saba, zalipotimu.

Akamwita mkwe, akamwitikia, labeka. Akamwambia, nna maneno matatu nataka kukwambia. Akamwambia, Bwana, Shekhi langu, licha ya matatu, hatta kumi na matatu, sijione hasara kunambia. Akamwambia, sina zayidi ya matatu haya. Akamwambia, Ee walla, nambie. Akamwambia, la kwanza, nataka unipe rukhusa, mimi na mke wangu kwenenda kwangu, la pili, sikasirike kwa haya nnaokwambia, la tatu, nataka unipe ruksa leo kabla ya kesho, kwani nimeona leo siku njema ya kutoka, mimi na mke wangu. Na wewe si nene, tumekimbia, utatuona ussubui na jioni, hatta labuda wewe mwenyewe ushibe, wewe, mwenyi kujiwa.