Page:Swahili tales.djvu/76

This page has been proofread.
56
SULTANI DARAI.

mwake, itakapokuwa siku kumi kwa siku moja, atapata kitu kununua paa? Lakini twende tukamtazame, Muhadimu, twende tukamtazame yule asharati anaosumbua nafsi yake kupiga kelele, na kukusumbua wewe mwenyi mzigo kitwani, ila twende tukamtazame atanunua kweli, kama hatanunua killa mtu atampiga bakora moja moja, apate kutubu, siku ya pili akimwona mtu na mzigo wake, asimwite.

Wakaenda hatta wakafika. Ah! hawa paa, nunua bassi, nataka paa, nataka paa, hawa, ewe maneno si kitendo. 'M! Utatamani kwa macho, hutashika kwa mkono.

Akamwambia muhadimu, Paa wako kiassi gani? Wakaruka wale watu watatu. Ee mwongo, Ewe unajua killa siku paa wanauzanya wawili kwa robo. Bassi, akamwambia, nataka mmoja kwa themuni. Ee mwongo wee, una themuni wee, umepata api? Akamtia mdukuo.

Wamenitilia nini, bwana, mdukuo burre? Nimekutendani? Nimekutukana, nimekufyonya? Nimekutwalia chako? Mimi namwita huyu mwenyi paa kununua hawa paa wake, mmetokea ninyi pingamizi, mwataka kuniharibia hii biashara, nisipate? Akashika utamvua wa nguo, akifungua ile themuni, akamwambia, twaa, muhadimu, nipe paa wangu mmoja nitazame. Akatwaa muhadimu yule paa. Huyu, bwana, chukua. Muhadimu akacheka yeye, mbona ninyi wenyi kanzu na vilemba, na panga na majambia, na viatu miguuni, nanyi ni wangwana wenyi mali, hamkosi, nanyi mmenambia, huyu ni fukara hohe hahe, hana mbele hana nyuma, naye ameweza kununua paa wa themuni, nanyi kuwa wangwana bora na mali kwenu tele hamkuweza kununua hatta nussu ya themuni,