Page:Swahili tales.djvu/86

This page has been proofread.
66
SULTANI DARAI.

sana kwa majani hayo, na mvili huo, na upepo wa hapo, gissi ulio mwema, tena na mto karibu, tena pana na faragha, hapana njia, hapana nyumba karibu, hatta mto wenyewe u katika magugu, na kesho nikiamka nitakwenda kuko huko.

Amwambia, ukiamka ukaende, bwana. Wakalala.

Hatta ussubui kulipopambauka akatoka paa mbio, akaenda zake, akakutana na watu yule paa—huyo, huyo, paa wa maskini mkamateni, huyo, huyo, kamateni paa wa maskini, kamateni, kamateni, wasimpate. Paa akakaza mbio, akaenda zake. Wale waliomfukuza wakarudi.

Hatta muda wa siku tano yule paa alipokwenda kulisha, akaenda palipo mti mkubwa, u katika miiba, u katika msitu, yule paa amechoka jua, akanena, pale penyi mti mkubwa nikajifiche hapo pale pana mvili nipumzike hili jua. Akaenda, akalala, pale penyi mti ule mkubwa. Muda mkubwa waliopita kulala kwake yule paa pale penyi mti mkubwa ule.

Akiamka akizungukazunguka chini ya mti ule, akaona pahali pamefanya majani kichungu, akainua mguu wake, akapekua, akaona almasi kubwa mno, inang'ara sana. Ooo yule paa akasangaa, haya ndio mali, hii ndio ufalme, lakini nikimpelekea bwana wangu hii, atauawa, kwani maskini ataambiwa, umepata api, akinena nimeokota hasadikiwi, hatta atakaponena nimepewa hasadikiwi, bassi ya nini miye kwenda kumtia bwana wangu katika matata? Ntatafuta watu wenyi nguvu, nao ndio wawezao kuila.

Akaondoka paa mbio, akaingia katika mwitu, naye almás