Page:Swahili tales.djvu/88

This page has been proofread.
68
SULTANI DARAI.

akaiuma kinwani, akaenda mbio sana katika mwitu asipate mji siku ile, akalala mwituni, hatta ussubui wa pili, akaondoka kabla ussubui haujapambauka, akaenda mbio hatta jua lalipokoma mafungulia ng'ombe makuu, akapumuzika, hatta lalipokoma jua vitwani akaenda zake mbio sána na almás yake kinwani, hatta jua lalipokuchwa akalala ndiani. Hatta ussubui walipopambauka, akaenda zake mbio akajitahili kwenda mbio sana hatta lalipokoma mafungulia ng'ombe madogo akapumzika akaona dalili za mji karibu akaenda zake mbio akaenda mbio sana, hatta lalipopinduka jua vitwani, akiona dalili ya majumba na mji asiweze kusimama tena, akakaza mbio sana akaenda hatta akiwasili katika njia kuu ya katika ule mji, na ile njia imekabili nyumba ya Sultani. Akaenda zake hatta akiona nyumba ya Sultani imefafanukia. Akazidi kukaza mwendo, na mle katika njia anapopita, watu wamesangaa, wamemwona paa mbio na kitu ndani ya majani amekiuma kinwani, amelekea nyumba ya Sultani.

Wale watu waliomo katika mji walisangaa hatta paa akiwasili pale mwangoni pa Sultani, na Sultani amekaa mbele ya mwango. Paa akapiga, hodi! hodi! Ameitupa chini almas, naye amekaa kitako pale njiani kinatweta, akapiga marra ya pili, hodi! hodi! Sultani akanena, sikilizeni hodi inaopigwa hiyo. Wakamwambia, bwana, hodi inapigwa na paa. Akawaambia mkaribisheni, mkaribisheni! Wakaenda watu watatu mbio, wamwambia, haya, ondoka, unakwitwa, karibu. Akaondoka paa, akainua ile almasi yake, hatta pale pa Sultani, akiiweka chini ya miguu ya Sultani.

Akamwambia, Bwana, Masalkheri. Sultani akamwitika, Allah masik bilkheri, karibu. Nimekaa, Bwana. Sultani akaamuru, asikari, leteni busati, leta na zulia, lete na