Page:Swahili tales.djvu/98

This page has been proofread.
78
SULTANI DARAI.

na kanzu moja ya daria ilio njema sana, akatoa na kikoi kimoja cha albunseyidi kilicho chema sana, akatoa na kitambi kimoja kariyati kilicho chema sana, akatoa na shatoruma ilio njema sana. Akaenda kuleta kitara kimoja kilicho chema sana cha thahabu. Akaenda akaleta jambia moja la temsi la thahabu lilio jema sana. Akaleta na jozi moja ya viatu, akapewa na bakora moja la mtobwi lilio jema sana.

Akamwambia paa, Chukua vitu hivi na waaskari hawa hatta kwa Sultani, mpe, apate kuja zake. Akamwambia, Ah! bwana, itayamkini kuchukua askari hawa, mimi kwenda kufazehi bwana wangu, na hapo alipo ni kama alivyozaliwa na mamaye? Mimi pekeyangu natosha, bwana.

Akamwambia, Utatoshaje wee pekeyako, na huyu ni frasi, na nguo hizi? Amwambia, Bwana huyu frasi nifungeni hapa shingoni pangu, na hizi nguo zifungeni juu ya mgongo wa frasi, mzifunge sana, kwani mimi nitakwenda mbio na frasi. Sultani akamwambia, Kama waweza nitakufanyia. Akamwambia, Bwana, kama siwezi singekwambia, hatta hakwambia naliweza.

Akafungia frasi shingoni pake, zikafungwa na nguo juu ya mgongo wa frasi. Akamwambia, Ah! bwana, kua heri, naenda zangu. Sultani akamwambia, Je! paa, tukungoje lini? Akamwambia, mshuko wa alasiri kasiri. Akamwambia, Inshallah.

Paa akatoka mbio na frasi wake, paa mbele, frasi nyuma. Wale watu waliomo mji ule, na Sultani, na maamiri, na mawaziri, na maakida, na makathi, na jamii wangwana walio nao matajiri katika mji, wakataajabu paa